Mkwamo

Author(s):
Published:
Availability :
In Stock
Mkazo na Kasuku hapo awali hawakushirikiana kama wafalme katika falme mbili za wasulenge na wapomboli zinazozungumziwa katika tamthilia hii. Shida zilizotokea hapo baadaye zikawafanya waungane ingawa...
UGX 8,000

Mkazo na Kasuku hapo awali hawakushirikiana kama wafalme katika falme mbili za wasulenge na wapomboli zinazozungumziwa katika tamthilia hii. Shida zilizotokea hapo baadaye zikawafanya waungane ingawa muungano wao haukuwasaidia kujisalimisha kutoka katika mkono wa Kovile kamanda wa kikoloni walipojaribu kutetea falme zao.

Masereka Levi Kahaika ambaye alizaliwa wilayani Bundibugyo magharibi mwa Uganda ni mhadhiri wa Isimu na Fasihi. Amefundisha katika shule na vyuo mbalimbali nchini Uganda. Ni mwandishi wa Mashairi, Riwaya, Hadithi fupi na ni mtafiti mashuhuri kuhusu kazi za uandishi wa kiuamilifu. Ni mwalimu aliye na tajriba kubwa katika ufundishaji wa Kiswahili. Ana Uzamili, shahada na stashahada katika Kiswahili. Hivi sasa anafundisha katika Chuo Kikuu cha Kyambogo- Kampala.

M.George Black T’songo ni mzaliwa wa Kasese. Ni mtunzi ambaye amebobea sana. Ni mwanajeshi katika Jeshi la ulinzi wa wananchi wa Uganda.

Bw. George na Masereka ni miongoni mwa waandishi chipukizi wa Kiswahili wanaojaribu kutegua kitendawili cha kutokuwepo waandishi wa kazi za kifasihi nchini Uganda.

-->